WANAWAKE WA TUWASA WASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2026 SIKONGE
09 Mar, 2026
Wanawake wa TUWASA wameshiriki maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa Wilayani Sikonge ambapo wanawake wa mkoa wa Tabora walikutana na kuadhimisha siku hii.

Maadhimisho hayo yalifanyika kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu isemayo: “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana; Msingi Jumuishi kufikia Dira ya Maendeleo 2050.” na yaliongozwa na Mgeni Rasmi Mhe. Upendo Wella akishirikiana na viongozi mbalimbali kutoka katika Wilaya zote za Tabora.

