TAARIFA YA UPUNGUFU...
TAARIFA YA UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI
15 May, 2026

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) inawafahamisha wateja wake kuwa, tarehe 16/05/2026 kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji unaotokana na KASHWASA kufanya matengenezo ya hitilafu katika pampu moja ya kusukuma maji ya ziwa Viktoria pamoja na TANESCO Tabora kufanya maboresho katika miundombinu yao ya umeme.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wote utakaojitokeza na tunawasihi wateja wetu kuhifadhi maji na kutumia kwa uangalifu mpaka matengenezo ya pampu na maboresho ya njia za umeme yatakapokamilika. 

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TUWASA
15/05/2026