TAARIFA YA KATIZO LA HUDUMA YA MAJI
02 May, 2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) inawafahamisha wateja wake kuwa kutakuwa na katizo la huduma ya maji linalotokana na Tangazo tulilotoa la KASHWASA kufanya Usafi katika Matanki, hata hivyo KASHWASA walipata changamoto ya umeme na kusababisha zoezi hilo kuchelewa. Usafi wa Matenki umekamilika jana jioni.
Tunawafahamisha wateja wetu kuwa Maji bado hayajafika katika tanki letu la Itumba. Hivyo huduma itarejea mara baada ya maji kujazwa katika tanki la Itumba.
Maeneo yanayoathirika ni;
- Kata ya Mtendeni
- Kata ya uyui
- Masagara
- Ikindwa
- Itonjanda
- Ifucha
- Ndevelwa
- Mtendeni
- Ipuli
- Isevya
- Malolo
- Ntalikwa
- Mlimani city
- Kipalapala
Tunaomba radhi kwa usumbufu wote uliojitokeza na tunawasihi wateja wetu kuhifadhi maji na kutumia kwa uangalifu mpaka huduma itakaporejea.
Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TUWASA
02/05/2026. Translate in english

