Historia

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) ni Mamlaka inayojiendesha kwa kutoa huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira. Ni miongoni mwa Mamlaka ishirini na sita za nchini Tanzania ambazo zilitangazwa na Waziri mwenye dhamana ya Maji tarehe 1 Januari 1998; kupitia mamlaka aliyopewa na Kifungu cha 38 cha Sheria ya Maji ya mwaka 1949 na Kanuni ya 3 (1) ya Kanuni za Maji iliyochapishwa katika Tangazo la Serikali Na. 371 la tarehe 25 Julai 1997.

Shughuli kuu za Mamlaka ni Kusambaza Majisafi na salama, utoaji wa huduma za usafi wa mazingira na kukusanya mapato ya uendeshaji na matengenezo katika maeneo yote ya huduma ikiwemo Manispaa ya Tabora, mji wa Sikonge, Urambo mjini na Isikizya Wilayani Uyui.