TAARIFA YA UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI
24 Apr, 2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) inawafahamisha wateja wake kuwa, tarehe 25.04.2026 kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji unaosababishwa na TANESCO kufanya maboresho katika miundombinu ya umeme.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wote utakaojitokeza na tunawasihi wateja wetu kuhifadhi maji na kutumia kwa uangalifu mpaka huduma itakapotengemaa.
Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma - TUWASA
24/04/2026

