TUWASA YAWANOA VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA NA VIJIJI.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TUWASA Bw. Dick Mlimuka ameongoza kikao kazi baina ya Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji ambapo mada mbalimbali zilitolewa na kufanyika majadiliano ya pamoja.

Mada zilihusisha Nguvu ya Mawasiliano na Utoaji taarifa kwa wakati, Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Manispaa ya Tabora, Umuhimu wa ushirikishwaji Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji na mada ya mwisho ilikua Usimamizi wa Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira namba 5 ya mwaka 2019.
Kwa ujumla mada zililenga kuimarisha mawasiliano na uhusiano, kukumbushana haki na wajibu, kufanya kazi kwa misingi ya Sheria ya maji na usafi wa mazingira namba 5 ya mwaka 2019 pamoja na kusimamia upatikanaji wa maji Manispaa ya Tabora hasa ikizingatiwa kuwa maji yapo ya kutosha.

Mwisho Mhe. Gullam Hussein D. Remtullah Mstahiki Meya Manispaa ya Tabora alifunga kikao kazi hiki muhimu kwa kuonesha imani yake kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji kuwa ni watu muhimu sana wachapa kazi na wanapenda maendeleo
" Nawahakikishia TUWASA kuwa Viongozi hawa tunawategemea sana ni wapenda maendeleo endeleeni kuwatumia katika huduma ya maji" Mhe. Gullam Hussein Dewji.
Mhe. Gullam aliwasisitiza Viongozi kuyatumia mafunzo waliyopewa kwa kuwa mabalozi wazuri kwenye maeneo yao ili TUWASA ifanye majukumu yake vizuri zaidi.

