WATUMISHI TUWASA USO KWA USO NA WATAALAM KUTOKA DAMU SALAMA NA TAKUKURU
Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA Mhandisi Mayunga A. Kashilimu amefungua mafunzo kwa watumishi wa TUWASA kuhusu Afya ya Akili na Masuala ya Rushwa.

Mtaalam kutoka TAKUKURU Bi. Happiness Madeghe alitoa mada kuhusu Rushwa ambapo alisisitiza ushirikiano wa jamii nzima katika kuzuia na kupambana na rushwa kwa kuwa rushwa ni kosa la jinai, kosa la kimaadili na pia ni kosa la kiimani. " Acha kutoa au kupokea rushwa" Happiness Madeghe

Pia watumishi walipata fursa ya kupata mafunzo kutoka kwa Daktari Juma Abdallah Kiangi na Bi. Nyawada Ernest Magesa wataalam kutoka Damu Salama (NBTS) kanda ya Magharibi Tabora.
Wataalam hao waliwekea mkazo umuhimu wa kutunza afya ya akili kutokana na madhara makubwa yaliyopo na ikitokea mtu ameathirika na changamoto ya afya ya akili ni vizuri akapewa ushauri nasaha mapema ili kuzuia madhara zaidi.
Na alihitimisha kwa kuwakumbusha umuhimu wa kuchangia damu " Changieni damu ni matendo ya huruma" Dkt. Juma Abdallah Kiangi.

Watumishi walijadili na kuuliza maswali kuhusu mada zikizowasilishwa na kupata uelewa wa pamoja.

