TUWASA YAFANYA KIKAO...
TUWASA YAFANYA KIKAO CHA TATHMINI YA UTENDAJI NA VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA NA VIJIJI MANISPAA YA TABORA.
20 Jan, 2026
TUWASA YAFANYA KIKAO CHA TATHMINI YA UTENDAJI NA VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA NA VIJIJI MANISPAA YA TABORA.

Mhe. Upendo Wella Mkuu wa Wilaya ya Tabora amefungua kikao kazi cha tathmini ya utendaji baina ya TUWASA na Viongozi Serikali za Mitaa na Vijiji Manispaa ya Tabora na kuagiza yafutayo.:

  1. TUWASA boresheni mawasiliano na viongozi wa serikali za Mitaa na Vijiji .
  2. Viongozi Serikali za Mitaa na Vijiji washiriki katika utunzaji wa vyanzo vya maji na miundombinu yake kwa kuwasimamia wanaowaongoza katika maeneo yao.
  3. Pia Viongozi wasimamie wanaowaongoza walipe bili za maji kwa wakati na wahimizwe kupanda miti.
  4. Aidha Mha. Mayunga Kashilimu Mkurugenzi Mtendaji TUWASA amewakumbusha viongozi kuwa maji yapo ya kutosha wajiunge na huduma, wasaidie kutoa taarifa za wizi wa maji na mivujo ya mabomba .
  5. Amehitimisha kuwa Viongozi wasaidie kuelimisha wadau wa maji kutumia maji safi na salama kutoka TUWASA na ameshukuru uongozi wa Mkoa, Wilaya na Manispaa ya Tabora kwa namna wanavyoshirikiana na TUWASA.