TUWASA IMESHIRIKI KI...
TUWASA IMESHIRIKI KIKAMILIFU MAADHIMISHO YA MEI MOSI 2026 - WILAYA YA KALIUA, TABORA
02 May, 2026
TUWASA IMESHIRIKI KIKAMILIFU MAADHIMISHO YA MEI MOSI 2026 - WILAYA YA KALIUA, TABORA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) imeshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) ngazi ya Mkoa yaliyofanyika katika Wilaya ya Kaliua, Tabora.

Mgeni Rasmi katika Maonyesho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Paul Matiko Chacha amewasihi Wafanyakazi kuendelea kuwa wavumilivu na kufanya kazi kwa Uadilifu na bidii wakati Serikali ikiendelea kuboresha Maslahi na Mazingira ya kazi kwa wafanyakazi. Aidha amepongeza namna serikali inavyoendelea kuhakikisha kusimamia upandaji wa vyeo na madaraja kwa wafanyakazi.

Amewataka watumishi kusikikiliza wananchi na kuwahudumia wakati wote,  halikadhalika kuzingatia kujiendeleza kielimu katika nafasi zao kama inavyopaswa. Amesihi jamii pia kuwatunza na kuwapatia watoto elimu bila ubaguzi kwa maendeleo ya Taifa.

Katika maadhimisho hayo zaidi ya wafanyakazi 500 walipokea vyeti vya mfanyakazi hodari ambapo TUWASA imechagua watumishi 3 hodari ambao walitunukiwa vyeti na kupokea zawadi ya pesa taslimu kila mmoja.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Mei Mosi 2026 ni "Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050" ambapo Kitaifa yamefanyika Mkoa wa Njombe na Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
#kaziiendelee kazinaututunasongambele. Translate in english