TUWASA YAENDESHA KAMPENI YA UTOAJI ELIMU KWA MAWAKALA WA MAGATI YA MAJI WILAYANI SIKONGE
30 Jun, 2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) inaendelea na utoaji wa elimu kwa Mawakala wa Magati kuhusu kuzuia upotevu wa maji, usimamizi sahihi wa magati ya maji kulingana na mikataba, ulipaji wa bili za maji kwa wakati sambamba na uainishaji wa bei elekezi ya maji katika Magati hayo ambayo ni shilingi 30 kwa ndoo ya lita 20

TUWASA inatoa wito kwa wananchi wote wanaotumia magati ya maji kununua maji kwa bei elekezi, aidha mwananchi asisite kutoa taarifa endapo atauziwa maji tofauti na bei elekezi.
Kazi hii imefanyika katika Magati yote ya Maji yaliyopo eneo la Sikonge.

