TAARIFA YA UPUNGUFU...
TAARIFA YA UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI
14 Aug, 2026

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) inawafahamisha wateja wake kuwa, tarehe 15/08/2026 kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji unaotokana na uwezekana wa kukosa umeme kwenye mitambo ya uzalishaji.

Huduma inatarajiwa kuimarika mara baada ya TANESCO kukamilisha matengenezo hayo na maji kujazwa katika matanki yetu.

TUWASA inaomba radhi kwa usumbufu wote utakaojitokeza na tunawasihi wateja wetu kuhifadhi maji na kutumia kwa uangalifu mpaka huduma itakapoimarika.

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TUWASA

14/08/2026