BARAZA LA WAFANYAKAZ...
BARAZA LA WAFANYAKAZI LIMEKETI KIKAO CHAKE LEO TAREHE 11.10.2023
11 Oct, 2023
BARAZA LA WAFANYAKAZI LIMEKETI KIKAO CHAKE LEO TAREHE 11.10.2023

Baraza la Wafanyakazi limeketi kikao chake Leo tarehe 11.10.2023 likiongozwa na Mwenyekiti Eng. Mayunga Antony Kashilimu akiwepo na mjumbe mmoja wa nje ambaye ni Katibu wa chama Cha Wafanyakazi (Tughe) Mkoa wa Tabora Bi. Amina Mwaluko.

 

Bi Amina (wa kwanza kushoto) ameipongeza Menejimenti ya TUWASA kwa namna ilivyoshiriki maadhimisho ya Meimosi, namna ilivyoboresha maslahi ya watumishi sambamba na kuwapa sare za kazi na ameshauri iendelee hivi hivi ili kuwatia moyo watumishi waweze kufikia malengo ya taasisi.

Mwenyekiti, Eng. Mayunga Antony Kashilimu (aliyekaa katikati) aliwataka wajumbe kuhakikisha wanahamasisha watumishi kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili kufikia malengo ya bajeti tunayojiwekea ambayo mwisho yatasaidia kutimiza malengo ya watumishi pia.

Mwisho aliwashukuru wajumbe kwa ushiriki wao na kutoa maoni yenye tija kwa Mamlaka na kusema vikao hivi ni vizuri vikawa vinafanyika na maeneo mengine Kama vile Urambo, Sikonge, Isikizya au maeneo ya vyanzo vya maji kwakuwa yote hayo ni maeneo ya TUWASA ya kutoa huduma ya majisafi na usafi wa Mazingira.