KAMATI YA SIASA YA W...
KAMATI YA SIASA YA WILAYA YA TABORA WAMEKAGUA MRADI WA MAJITAKA UNAOTEKELEZWA ENEO LA MIRAMBO BARRACKS.
28 Jun, 2023
KAMATI YA SIASA YA WILAYA YA TABORA WAMEKAGUA MRADI WA MAJITAKA UNAOTEKELEZWA ENEO LA MIRAMBO BARRACKS.

Kamati ya Siasa ya Wilaya ikiongozwa na Ndugu Mohamed Katete Mwenyekiti wa  kamati hiyo wamekagua Mradi wa Majitaka unaotekelezwa eneo la Mirambo barracks wenye thamani ya shilingi  Bilioni 1.6 na utekelezaji wake umefikia asilimia 10.

Aidha Mwenyekiti amempongeza Mhandisi Kashilimu Mayunga Mkurugenzi Mtendaji wa Tuwasa kwa utekelezaji wa Mradi huo na pia ushirikishwaji wa Mradi kwa wadau mbalimbali. Ameagiza mradi utekelezwe kwa wakati kama ilivyopangwa na kiwango kinachotakiwa.