Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) wameshiriki maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi-2025
01 May, 2025

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) wameshiriki maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi yaliyofanyika kimkoa Uwanja wa Samora Wilayani Nzega.
Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watumishi wote wa TUWASA tunawapongeza watumishi watatu waliokua wafanyakazi hodari kwa mwaka 2025.
Wafanyakazi hao ni Bw. Mrisho M. Mdumla - Fundi mchundo mwandamizi (Kushoto), Bw. Evans E. Binya - Meneja wa kanda ya Sikonge (Katikati), na Bi Sarafina S. Rwezimula - Mwendesha Mitambo.