MRADI WA UBORESHAJI...
MRADI WA UBORESHAJI HUDUMA YA MAJI SIKONGE SASA ASILIMIA 89
20 May, 2026
MRADI WA UBORESHAJI HUDUMA YA MAJI SIKONGE SASA ASILIMIA 89

Mradi unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) wa Uboreshaji Huduma ya Maji Sikonge sasa umefikia 89% ya utekelezaji wake.

Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 1.59 ambao unaendelea, unahusisha ununuzi wa Mabomba ya vipenyo vya kuanzia 25mm hadi 200mm na viungio vyake kwa jumla ya kilomita 41, ununuzi wa mita za maji, uchimbaji na ufukiaji wa mitaro pamoja na ujenzi wa chemba katika maeneo ya Kata ya Mission eneo la Usupolo na Usega, Stendi mpya, Majengo, New fashion na Ukanga ambao unaenda kuboresha hali ya huduma ya maji kwa wakazi wa Sikonge mjini.

Akikagua hatua ya utekelezaji wa Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA Mha. Mayunga Kashilimu akiambatana na Meneja wa TUWASA - Sikonge Evans Binya ametembelea eneo la Majengo, New fashion na Masinge ambapo mradi huo unaendelea kutekelezwa. Amesema hatua ya utekelezaji wa Mradi ni nzuri, na amesisitiza kuzingatia kukamilisha mradi kwa wakati ili uweze kuwanufaisha wananchi.

Mradi huu umetatua changamoto ya kubwa ya huduma ya maji kwa wakazi wa eneo la Majengo Sikonge, ambao awali hawakuwahi kufikiwa na huduma ya maji, na sasa wananufaika na mradi huo. Mradi unatarajia kunufaisha zaidi ya wakazi 12500