MRADI WA MAJITAKA KW...
MRADI WA MAJITAKA KWA MIJI 10 KUANZA
17 Aug, 2023
MRADI WA MAJITAKA KWA MIJI 10 KUANZA

Eng. Mayunga A. Kashilimu (Aliyesimama), Mkurugenzi Mtendaji TUWASA amewatambulisha wahandisi washauri wa WWSP na LUPTAN ambao wameambatana na Eng. Loishinye Ngotee kutoka Wizara ya Maji katika uongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kwa ajili ya kuanza kazi ya upembuzi yakinifu, usanifu wa mradi wa majitaka pamoja na kuandaa nyaraka za zabuni.

Mradi huu unahusisha miji 10 ya makao ya mikoa ambayo ni Singida, Tabora, Mpanda, Kahama,Sumbawanga,Kigoma, Geita, Njombe, Mtwara na Lindi.