TEHAMA ILIVYOLETA MA...
TEHAMA ILIVYOLETA MATOKEO CHANYA KWA WATEJA WA TUWASA
15 Feb, 2024
TEHAMA ILIVYOLETA MATOKEO CHANYA KWA WATEJA WA TUWASA

Bw. Hussein Mnete ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA TUWASA ameeleza kuwa mabadiliko ya Teknolojia yamekuwa chachu ya maendeleo kwakuwa mambo mengi yamerahisishwa  kwa wateja ikiwepo;-

  • Usomaji wa mita , uchakataji wa taarifa na usambazaji wa bill hufanywa kwa kutumia mfumo maalum hivyo mteja anapata usomaji wake haraka kupitia simu yake ya mkononi baada ya kusomewa na bill yake pia.
  • Wateja wanaweza kujihudumia wenyewe kwa kupitia mifumo mbalimbali ili kuweza kuangalia madeni yao na kulipa bill zao popote walipo mfano *152*00# kwa simu ya mkononi unaweza kuona deni lako na kulipia pia.
  • Wateja wanaweza kuhabarishwa taarifa mbalimbali kutoka TUWASA kwa kupitia tovuti ya Mamlaka ambayo ni www.tuwasa.go.tz au mitandao ya kijamii Instagram, Facebook ,makundi sogozi na kupitia simu za mkononi.

Aidha amewatahadharisha wateja kuwa waangalifu kwa kuhakikisha malipo yote ya huduma ya maji wanafanya kwa kutumia namba ya malipo inayotolewa TUWASA  na kufanya malipo kwa simu zao, wakala wa benki au benki sio kumtumia mtu pesa kwa namba binafsi.

Mwisho Bi Najibah Batenga  amewaomba wadau wa maji kupenda mabadiliko ya teknolojia ili kwenda sambamba na huduma zinavyoboreshwa, kujihudumia na upashanaji wa habari kwakuwa TUWASA inatarajia kuweka huduma zote za maji kidijiti.