Mhe. JUMAA AWESO WAZ...
Mhe. JUMAA AWESO WAZIRI WA MAJI ATOA MILIONI 500 KUKAMILISHA MRADI WA MAJI MIJI 28 URAMBO NA MILIONI 400 MRADI WA BWAWA LA MAJI URAMBO.
08 Feb, 2026
Mhe. JUMAA AWESO WAZIRI WA MAJI ATOA MILIONI 500 KUKAMILISHA MRADI WA MAJI MIJI 28 URAMBO NA MILIONI 400 MRADI WA BWAWA LA MAJI URAMBO.

Waziri Aweso amefika Mkoani Tabora na kuzungumza na watumishi wa sekta ya maji Tabora katika ofisi ya Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Tabora (TUWASA) ambapo amesisitiza kuzingatia uhusiano mzuri na wadau wa maji. Ameyasema hayo akiwa anajiandaa kufanya ukaguzi wa mradi wa maji wa miji 28 akiwa ameambatana na eng. Mwajuma Waziri Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

Baada ya kupata taarifa ya hali ya usambazaji maji, utekelezaji wa miradi ya maji  na kukagua miradi hiyo  aliagiza mradi wa miji 28 ukamilike ifikapo mwisho wa mwezi Februari, 2026 wananchi waanze kupata maji sambamba na kukamilika kwa bwawa la maji la Urambo linalosimamiwa na RUWASA.

Aidha baada ya kuelezwa changamoto zilizopo ameahidi kutoa shilingi milioni 500 kukamilisha mradi wa miji 28 wananchi wapate huduma ya maji Urambo sambamba na kutoa shilingi milioni 400 kukamilisha bwawa la maji la Urambo lililofikia utekelezaji wa asilimia 88.

Ikumbukwe kuwa katika utekelezaji wa mradi wa maji miji 28 tayari Sikonge wananufaika na maji kutoka Ziwa Victoria kupitia mradi huo.