WATAALAM KUTOKA WIZA...
WATAALAM KUTOKA WIZARA YA MAJI, WATEMBELEA MRADI WA MAJITAKA UNAOTEKELEZWA TABORA.
07 Sep, 2023
WATAALAM KUTOKA WIZARA YA MAJI, WATEMBELEA MRADI WA MAJITAKA UNAOTEKELEZWA TABORA.

Leo tarehe 07.09.2023 Wataalam kutoka Wizara ya Maji, Eng. Selemani Ziota (wa pili kutoka kulia) na Eng. Fatma Omary (wa pili kutoka kushoto) wamepata maelezo kuhusu utekelezaji wa mradi wa majitaka unaotekelezwa Tabora.

Meneja mradi, Eng. Amagore Ngofira (wa kwanza kushoto) ameeleza kuwa mradi umefikia  asilimia 16 ya utekelezaji, endapo utakamilika utasaidia kwa kiasi kikubwa huduma ya usafi wa Mazingira Tabora.

Aidha wataalam hao wamesema watafuatilia malipo ya mkandarasi ili mradi utekelezwe kwa haraka na kuleta matarajio yaliyokusudiwa kwa wakaazi wa Tabora.

Mwisho kabisa Eng. Juma Kasekwa (wa kwanza kulia) aliwashukuru wataalam hao kwa kutembelea mradi huu na kuahidi kuusimamia vema ulete matokeo chanya kama inavyotarajiwa.