WATAALAM KUTOKA WIZA...
WATAALAM KUTOKA WIZARA YA MAJI, WATEMBELEA WILAYA YA KALIUA MKOANI TABORA TAREHE 28/08/2023
31 Aug, 2023
WATAALAM KUTOKA WIZARA YA MAJI, WATEMBELEA WILAYA YA KALIUA MKOANI TABORA TAREHE 28/08/2023

Wataalam kutoka Wizara ya Maji wakiongozwa na Eng. Agripina Mashila Geodfrey (wa kwanza kushoto) wamefika TUWASA kwa ajili ya kufanya tathmini ya Hali ya huduma ya maji Kaliua ili kutekeleza agizo la Waziri wa Maji la kuifanya Kaliua kusimamiwa na TUWASA kisheria baada ya kutangazwa katika gazeti la Serikali.

Aidha wataalam hao, wakiongozana na watumishi kutoka TUWASA na RUWASA walifika kujitambulisha katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora, Mkuu wa Wilaya Kaliua, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kaliua na kutembelea ofisi ya Jumuiya ya watumia maji ya Kaliua ili kupata taarifa ya utendaji.

Baada ya tathmini kukamilika, taratibu za kisheria zitafuatwa kwa ajili ya makabidhiano rasmi ya Kaliua kusimamiwa na TUWASA.