ENG. MAYUNGA KASHILI...
ENG. MAYUNGA KASHILIMU, MKURUGENZI MTENDAJI WA TUWASA AMETEMBELEA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI WA MIJI 28.
02 Oct, 2023
ENG. MAYUNGA KASHILIMU, MKURUGENZI MTENDAJI WA TUWASA AMETEMBELEA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI WA MIJI 28.

Eng. Mayunga Kashilimu, Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA (aliyesimama katikati) ametembelea utekelezaji wa mradi wa maji wa Miji 28 ambapo ameambatana na Wataalam wengine kutoka TUWASA ambao ni Bi. Jamila Said ambae ni Mhasibu na Bw. Adam Shauri ambae ni msimamizi wa Mradi katika Kijiji Cha Ulimakafu.

Katika Kijiji Cha Ulimakafu utekelezaji wa mradi unafanyika ambapo uchimbaji wa mtaro umeanza na ulazaji wa bomba lenye ukubwa wa mm 500 aina ya steal pipe limeanza kulazwa.

Ameeleza msimamizi wa Mradi kuwa bomba hili linatoka Manispaa ya Tabora kuelekea Urambo na mara mradi utakapokamilika kabla ya mwaka 2025 wananchi wa Urambo watapata maji ya kutosha na kuondokana na adha ya maji iliyopo kwasasa kwakuwa maji yaliyopo sio ya uhakika ni ya visima ambavyo wakati wa kiangazi hupungua kina cha maji.