TAARIFA YA KATIZO LA HUDUMA YA MAJI
01 Apr, 2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) inawafahamisha wateja wake kuwa, tarehe 02/04/2026 kutakuwa na katizo la huduma ya maji.
Katizo hilo litasababishwa na TUWASA kufanya Matengenezo ya ufungaji wa valve katika bomba lenye kipenyo cha 8" na 6" katika barabara ya Ulaya.
Matengenezo hayo yataanza muda wa saa 1:00 asubuhi na yanatarajiwa kukamilika muda wa saa 6 mchana.
Maeneo yatakayoathirika ni;
1. Kariakoo
2. Kipalapala
3. National
4. Kata ya cheyo
5. Kiyungi
Tunaomba radhi kwa usumbufu wote utakajitokeza na tunawasihi wateja wote kuhifadhi Maji na kutumia kwa uangalifu mpaka huduma itakaporejea.
Imetolewa na ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TUWASA.
01/04/2026

