TAARIFA YA UPUNGUFU...
TAARIFA YA UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI
02 Nov, 2026

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) inawafahamisha wateja wake kuwa, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji tarehe 03/11/2026 unaotokana na katizo la umeme katika kituo cha kuzalishia maji cha Igombe.

Katizo hili limetokana na Tangazo la TANESCO la kufanya maboresho katika Miundombinu ya umeme kuanzia tarehe 2 - 8 Novemba 2026.

Hali hii itasababisha athari katika uzalishaji maji na usambazaji. Huduma itaimarika mara baada ya umeme kurejea na matanki kujazwa maji ya kutosha.

TUWASA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza na tunawasihi wateja wetu kuhifadhi maji na kutumia kwa uangalifu mpaka huduma itakapoimarika. Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TUWASA 02/11/2026