TAARIFA YA UPUNGUFU...
TAARIFA YA UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI
28 Oct, 2026

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) inawafahamisha wateja wake kuwa, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji tarehe 28/10/2026 na 29/10/2026 unaotokana na katizo la umeme katika kituo cha kuzalishia maji cha Igombe na kituo cha KASHWASA cha Ihelele

Katizo hili limetokana na Tangazo la TANESCO la kufanya maboresho katika Miundombinu ya umeme kuanzia tarehe 26 Oktoba mpaka tarehe 1 Novemba 2026 pamoja na maboresho katika miundombinu ya umeme kwa upande wa KASHWASA.

Hali hii imesababisha athari katika uzalishaji maji na usambazaji kwa mkoa wa Tabora.

Huduma itaimarika mara baada ya umeme kurejea na matanki kujazwa maji ya kutosha.

TUWASA inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na tunawasihi wateja wetu kuhifadhi maji na kutumia kwa uangalifu mpaka huduma itakapoimarika.

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TUWASA
28/10/2026