TAARIFA YA UPUNGUFU...
TAARIFA YA UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI
29 Oct, 2026

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) inawafahamisha wateja wake kuwa, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji siku ya Jumamosi tarehe 31/10/2026 unaotokana na katizo la umeme katika kituo cha kuzalishia maji cha Igombe. Katizo hili limetokana na Tangazo la TANESCO la kufanya maboresho katika Miundombinu ya umeme kuanzia tarehe 26 Oktoba mpaka tarehe 1 Novemba 2026.

Hali hii itasababisha uzalishaji maji na usambazaji kuathirika.

Maeneo yanayoathirika ni Kata za Kiloleni, Mapambano, Misha, Kabila, Kalunde, Tumbi, Tambukareli na Gongoni.

Aidha katika kata nyngine za mjini masaa ya usambazaji maji yatapungua. Huduma itaimarika mara baada ya umeme kurejea na matanki kujazwa maji ya kutosha.

TUWASA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza na tunawasihi wateja wetu kuhifadhi maji na kutumia kwa uangalifu mpaka huduma itakapoimarika.

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TUWASA 29/10/2026