MENEJIMENTI YA TUWASA YAKAGUA KITUO CHA KUZALISHA MAJI KAZIMA
30 Sep, 2026
Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) imetembelea na kukagua kituo cha kuzalisha maji cha Kazima lengo ni kuona hali ya uzalishaji maji na namna ambavyo kinaweza kuboreshwa kukiongezea uwezo wa kuhudumia wakazi wengi zaidi, pia kuangalia namna ambavyo Chanzo hicho kinaweza kudhibitiwa kuepusha madhara yanayoweza kujitokezaa kutokana na mvua kubwa za Elnino zinazotarajiwa kunyesha siku za karibuni.
Kituo cha Kazima kwa sasa kina uwezo wa kuzalisha lita 1,250,000 kwa siku na kinahudumia baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Tabora.

