MRADI WA UBORESHAJI...
MRADI WA UBORESHAJI WA BOMBA KUU LA MAJI KUT0KA UTYATYA KWENDA TANKI LA USAMBAZAJI MJINI SIKONGE UMEWEKWA JIWE LA MSINGI NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2026
22 Sep, 2026
MRADI WA UBORESHAJI  WA BOMBA KUU LA MAJI KUT0KA UTYATYA KWENDA TANKI LA USAMBAZAJI MJINI SIKONGE UMEWEKWA JIWE LA MSINGI NA  KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2026

Mradi wa Uboreshaji wa bomba kuu la maji. kutoka Utyatya kwenda tanki la Usambazaji wenye thamani ya shilingi 976,066,880 umewekwa jiwe la msingi na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 Ndg. Wazo Michael Mwang'onda tarehe 22/09/2026.

Mradi huu ambao umefikia asilimia 80 ya utekelezaji wake, umelaza bomba la 110mm kwa urefu wa mita 13,020 ambalo linategemewa kusaidia kufanya huduma kuwa endelevu mjini Sikonge, pale zinazopotokea dharula katika miundombinu ya maji ya ziwa Victoria.

Mwang'onda ameeleza kazi kubwa iliyofanywa na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuboresha huduma ya maji nchi nzima, kwamba Serikali imetumia gharama kubwa sana kuwafikishia huduma ya maji wananchi hivyo ni jukumu letu kuilinda miundombinu ya maji na kuitunza, aidha ameeleza kufurahishwa na utekelezaji wa mradi huu wa maji halikadhalika amewasihi wananchi kuendelea kuimarisha amani na utulivu.

Sikonge ni moja ya Miji ya awali kabisa Tabora kunufaika na maji ya Ziwa Viktoria. Kukamilika kwa mradi huu kutaiwezesha wakazi wa Sikonge kupata ongezeko la maji kwa kiwango cha mita za ujazo 720 kutoka bwawa la Utyatya.