TAARIFA YA TUWASA KW...
TAARIFA YA TUWASA KWA KAMATI YA SIASA YA CCM WILAYA TBR MANISPAA- 22.03.2024
22 Mar, 2024 Pakua

MAELEZO YA HUDUMA KWA UFUPI

TUWASA ni kifupi cha maneno “Tabora Urban Water supply and Sanitation Authority” ambayo ina jukumu la kutoa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwenye Manispaa ya Tabora pamoja na Miji ya Sikonge, Urambo, Uyui (Isikizya) na Kaliua.

1.1 Huduma ya Majisafi

  1. Chanzo cha maji kwa Mji wa Tabora ni Bwawa la Igombe na Ziwa Victoria ambavyo vyote vina uwezo wa kuzalisha maji jumla ya lita 57,842,000 kwa siku. Maji hayo yanatosheleza mahitaji ya Manispaa ya Tabora hadi mwaka 2045 (WAPCOS, 2015). Bwawa la Igombe pekee lina uwezo wa kuzalisha lita 30,000,000 kwa siku na miundombinu ya Ziwa Viktoria imesanifiwa kuleta maji Tabora Manispaa lita 27,842,000 kwa siku.
  2. Mahitaji ya maji kwa Manispaa ya Tabora ni lita 35,130,000 kwa siku ikijumuisha Miji ya Urambo, Sikonge, Uyui (Isikizya) na Kaliua. Hata hivyo, kutokana na ufinyu wa mitandao ya mabomba kwenye Miji ya Sikonge, Urambo na Kaliua na kutokuwepo maji ya kutosha kwenye maeneo hayo, uzalishaji halisi wa maji kwa sasa ni lita 19,500,000 tu kwa siku.
  3. Upatikanaji wa huduma ya maji katika Manispaa ya Tabora na Mji wa Isikizya (Makao makuu ya Wilaya ya Uyui) imefikia 95%. Makao Makuu ya Wilaya ya Sikonge ni 40.5%, Urambo ni 24.5% na Kaliua ni 26%. Maeneo ya Urambo, Sikonge na Kaliua yapo kwenye mradi wa Miji 28 ambao utekelezaji wake umeanza mwezi Aprili, 2023 na umefikia 32% hadi Januari, 2024. Mradi huo umepangwa kukamilika mwezi Oktoba, 2025. Baada ya kukamilika kwa mradi huo, upatikanaji wa maji kwa Miji ya Sikonge, Urambo na Kaliua utafikia zaidi ya 95%.
  4. Manispaa ina jumla ya Kata 29. Kata 28 zimefikiwa na mtandao wa mabomba na Kata 1 ya Ikomwa iko kwenye mradi wa quick win ambao unaendelea. Awali, ulipangwa kukamilika mwezi mwezi Machi, 2024 lakini kutokana na kuchelewa kwa malipo, mradi huo umeongezwa muda hadi Juni, 2024.
  5. Upatikanaji wa maji katika Manispaa ya Tabora ni wastani saa 22 kila siku, na Miji ya Sikonge, Urambo na Kaliua inapata maji kwa wastani wa saa 7 hadi 9 kwa siku.
  6. TUWASA ina jumla ya wateja 35,485 (Februari, 2024) na unit moja (lita 1,000 au ndoo 50 za lita 20 kila moja) ya maji inauzwa kwa shilingi 1,950 tangu mwezi Machi, 2022.
  7. Urefu wa mtandao wa Maji umefikia kilomita 1.288.2 kwenye maeneo yote ya utendaji ya TUWASA. Aidha, uwezo wa kuhifadhi maji ni mita za ujazo 24,490.