VIJANA WENYE MAHITAJ...
VIJANA WENYE MAHITAJI MAALUM WAMETEMBELEA BANDA LA TUWASA KATIKA MAONESHO YA NANENANE YANAYOFANYIKA VIWANJA VYA IPULI TABORA
07 Aug, 2024
VIJANA WENYE MAHITAJI MAALUM WAMETEMBELEA BANDA LA TUWASA KATIKA MAONESHO YA NANENANE YANAYOFANYIKA VIWANJA VYA IPULI TABORA

Vijana wenye mahitaji maalum wametembelea banda la TUWASA katika maonesho ya Nanenane na kupata elimu kuhusu uzalishaji wa maji ambapo wameuliza maswali likiwemo sababu ya kupata maji kidogo au kukatika kwa huduma ya maji katika Chuo chao cha Ufundi Rwanzali Tabora.

Ndugu Saimon Maganga aliwaeleza sababu za kupata maji kidogo au kukatika kwa huduma kunaweza kuwa na visababishi vingi kama vile mita ya maji kuziba, kusitisha uzalishaji kwa sababu ya matengenezo, kukatika kwa umeme au mabomba kupasuka.

Vijana hao walikiri kuelewa ufafanuzi uliotolewa na kusema wataendelea kuwa wanajifunza kuhusu huduma ya maji kwani maji ni hitaji muhimu sana kwao.