WAZIRI WA MAJI MHE....
WAZIRI WA MAJI MHE. JUMAA AWESO (MB) AMEFUNGUA MKUTANO WA WATAALAM WA RASILIMALI WATU NA UTAWALA, MAENDELEO YA JAMII NA MAAFISA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA KATIKA SEKTA YA MAJI
15 Nov, 2024
WAZIRI WA MAJI MHE. JUMAA AWESO (MB) AMEFUNGUA MKUTANO WA WATAALAM WA RASILIMALI WATU NA UTAWALA, MAENDELEO YA JAMII NA MAAFISA MAWASILIANO NA UHUSIANO KWA UMMA KATIKA SEKTA YA MAJI

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (mb) amefungua mkutano wa wataalam wa Rasilimali watu na Utawala, Maendeleo ya jamii na Maafisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma katika sekta ya Maji Novemba, 2024 jijini Dar es salaam.

Katika ufunguzi huo amewataka wataalam hao kuhakikisha wanatimiza jukumu la kumtua mama ndoo ya maji kichwani kwa kufikia asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini licha ya kazi kubwa ambayo imeshafanyika.

Amewataka wataalam hao kufanya kazi kwa bidii, weledi, kufuata Sheria na Taratibu pamoja na kutumia busara ili watumishi wapate morali ya kufanya kazi na kufikia malengo ya Taasisi ambayo ni kutoa huduma  bora zaidi.

Amesisitiza mnaposimamia maadili na nidhamu hakikisheni nanyi pia mnaonesha mfano " Mhe. Jumaa Aweso".

Amesema anatambua jitihada zinazofanywa na wataalam hawa licha ya changamoto zilizopo na amesisitiza umuhimu wa maafisa mawasiliano na maendeleo ya jamii kwakuwa ni nguzo muhimu ya kuunganisha wateja na Taasisi hivyo watoe taarifa za miradi wananchi wajue kazi zinazofanyika.

Mwisho amewapongeza na kuwashukuru wataalam hawa kwa kazi wanazofanya  na amewataka waendelee kufanya kazi kwa bidii.