ZIARA YA KAMATI YA S...
ZIARA YA KAMATI YA SIASA YA MKOA KATIKA MRADI WA MAJI MIJI 28 KWA MIJI YA SIKONGE, URAMBO NA KALIUA MKOA WA TABORA.
24 Jul, 2023
ZIARA YA KAMATI YA SIASA YA MKOA KATIKA MRADI WA MAJI MIJI 28 KWA MIJI YA SIKONGE, URAMBO NA KALIUA MKOA WA TABORA.

Ndugu Hassan Wakasuvi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu tarehe 19.07.2023 ameiongoza Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Tabora katika kukagua utekelezaji wa Mradi wa maji wa  Miji 28 katika eneo ambalo bomba kutoka Ziwa Victoria (taping point) litaungwa kwa ajili ya kupeleka maji Sikonge, Urambo na Kaliua mkoani Tabora.

Mhandisi Mayunga A. Kashilimu Mkurugenzi Mtendaji TUWASA ameeleza mbele ya Kamati hiyo kwamba Mradi huu umeanza kutekelezwa 11.04.2023, unatarajiwa kukamilika 10.10.2025 na baada ya kukamilika Wilaya zote saba za Tabora zitakuwa zinapata maji kutoka Ziwa Victoria ukilinganisha na sasa ambapo Wilaya 4 ndio zinapata maji hayo. Mradi huu unashirikisha watumishi kutoka TUWASA, RUWASA na Msimamizi mkuu ni Wizara ya maji.

Aidha Mhandisi Edward Tindwa  ambaye ni Msimamizi wa Mradi huu kutoka Wizara ya maji alieleza kuwa, Mradi huu unagharimu fedha kiasi cha shilingi Bilioni 143.26 na utakapokamilika unatarajia kuhudumia wakaazi 490,000 wa Sikonge, Urambo na Kaliua pamoja na Vijiji 56 vinavyopitiwa karibu  na bomba kubwa pamoja na kuzalisha maji lita 24,760 ambazo zitatosheleza mahitaji hadi mwaka 2040.

Ameeleza kazi zitakazofanyika ni pamoja na ujenzi wa matenki matano(5) katika miji hiyo na ulazaji wa mabomba.

Ndugu Hassan Wakasuvi Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Tabora ameagiza kwamba maeneo yote ambayo bomba linapita uandaliwe utaratibu wa maridhiano endapo itatakiwa walipwe fidia wananchi basi ni vema walipwe kwakuwa wanahamu sana na Mradi huu,  ni muhimu sana mawasiliano kuhusu utekelezaji wa mradi huu yaboreshwe baina ya wahusika wote kama vile ofisi ya Mkuu wa Mkoa, TARURA, TUWASA, RUWASA, TANESCO n.k

Mhandisi Edward Tindwa ameeleza kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na Kamati ikiwepo kukamilisha Mradi kwa muda uliopangwa.

“Bomba la Maji ni Siasa, nina imani mtatekeleza vema Ilani ya Chama cha Mapinduzi kupitia mradi huu na nina watakia kila lakheri” Ndugu Hassan Wakasuvi.