UTEKEKEZAJI WA MRADI WA MAJI WA MIJI 28 KWA MIJI YA SIKONGE, URAMBO NA KALIUA - TABORA WAFIKIA ASILIMIA 50.
Eng. Mayunga A. Kashilimu - Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA ametembelea na kukagua mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda miji ya Sikonge , Urambo na Kaliua unaotekelezwa na Mkandarasi Megha Engineering.
Amesema Mradi huu umetekelezwa na kufikia asilimia 50 na kuna matarajio makubwa ya kukamilika kama ilivyo katika mkataba wa ujenzi wa mradi huu unaotarajiwa kukamilika 2025 ameeleza Eng Mayunga.
Ameendelea kueleza matarajio makubwa yaliyopo baada ya kukamilika kwa mradi huu mkubwa unaogharimu fedha kiasi cha zaidi ya bilioni 143 kwamba utafanya upatikanaji wa maji kwa Sikonge, Urambo na Kaliua kuwa zaidi ya asilimia 90 na wakaazi 490,000 watapata huduma ya majisafi na salama ukilinganisha na sasa ni asilimia chini ya 50 ya upatikanaji wa maji kwa maeneo hayo.
Ameishukuru Wizara ya Maji na Serikali ya awamu ya sita kwa kuhakikisha fedha zinapatika na kutekeleza mradi huu ambao ni mkombozi wa upatikanaji wa huduma ya maji Sikonge, Urambo na Kaliua.