UPUNGUFU WA MAJI MAN...
UPUNGUFU WA MAJI MANISPAA YA TABORA KUISHA KESHO TAR 29/05/2024
28 May, 2024
UPUNGUFU WA MAJI MANISPAA YA TABORA KUISHA KESHO TAR 29/05/2024

Ameeleza Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA Mhandisi Mayunga Kashilimu kupitia kipindi cha Redio CG FM leo tarehe 28.05.2024 kuwa changamoto ya maji kutoka Ziwa Victoria iliyodumu kwa muda wa wiki nzima inaisha kesho na wakazi wa Manispaa ya Tabora na maeneo ya Isikizya watapata maji ya kutosha.

Ameeleza changamoto ilisababishwa na kupasuka kwa bomba kubwa la kutoa maji Ziwa Victoria Kupeleka katika tenki kubwa la Mabale lililopo Mwanza hivyo kuleta changamoto ya kusambaza maji ambayo yanafika hadi Tabora.

Hadi sasa matengenezo yamekamilika na maji yameanza kufika maeneo mengine ya Shinyanga na Kahama jambo ambalo linaashiria maji hayo kufika Tabora na kusambazwa kwa wateja kesho.

Biswalo Benard ambaye ni Mkurugenzi huduma kwa wateja pamoja na Mhandisi Juma Kasekwa ambaye ni Mkurugenzi Uzalishaji na Usafi wa mazingira wameeleza mpango wa kuunga bomba la maji kutoka Igombe kuja tenki la Itumba ili kusaidia wakati wa changamoto ya maji kutoka Ziwa Victoria na pia wamesisitiza wananchi kulipia bili zao za maji kwa wakati sambamba na madeni ili kuepuka usumbufu wa kupelekwa katika vyuombo vya sharia ambapo baadhi ya wadaiwa wameshafikishwa katika vyombo hivyo.

Kwa kuhitimisha Najibah Batenga ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano amewaomba wateja kuendelea kuboresha mawasiliano na TUWASA kuhusu huduma ya maji ili kuhakikisha wateja wanapata huduma bora na kuwajibika kuilipia pia.