UFAHAMU MKATABA WA H...
UFAHAMU MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA – TUWASA
23 Nov, 2023
UFAHAMU MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA – TUWASA

Katika kipindi cha Meza Huru kinachorushwa kupitia Redio V.O.T Ndugu Benard Biswalo – Mkurugenzi Huduma kwa Mteja ameuelezea Mkataba wa huduma kwa Mteja kuhusu Wajibu na Haki za Mtoa huduma na Mtumia huduma kwa kusisitiza pande zote kuhakikisha wanatimiza wajibu na kupata haki kama vile kutoa huduma bora bila upendeleo, kutoa taarifa zinazohusu huduma ya maji, kutoa elimu kwa wateja na kwa ujumla kujenga mahusiano mazuri na wateja.

Kwa upande wa wateja wana wajibu wa kulipa Ankara kwa wakati, kutoa ushirikiano kwa watumishi wa Mamlaka wanapohudumiwa, kulinda na kutunza miundombinu ya maji, kutoa maoni kuhusu huduma ya maji.

Aidha ameendelea kueleza kwamba TUWASA tupo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa Tabora ambao ndio waajiri wetu na hatuna haja ya kunyanyua mabega ila kuwanyanyua wananchi kwa kila upande kutimiza wajibu wake ikiwepo kulipia Ankara za maji kwa wakati na kupata huduma bora  na endelevu.

Mwisho kabisa Bi Najibah Batenga amewasisitiza wateja kutimiza wajibu wao ili wapate haki yao na pia amewaomba wananchi kufuatilia taarifa mbalimbali katika tovuti na mitandao ya kijamii Facebook na Instagram kwa kuwa taarifa nyingi zinatolewa humo ikiwepo uwepo wa mkataba wa huduma kwa mteja katika Tovuti ya TUWASA.