TUWASA YAPONGEZWA MA...
TUWASA YAPONGEZWA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST KATIKA MRADI WA MAJISAFI NA SALAMA WA SHILINGI MILIONI 601,868,971.
20 Aug, 2024
TUWASA YAPONGEZWA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST KATIKA MRADI WA MAJISAFI NA SALAMA WA SHILINGI MILIONI 601,868,971.

Ndugu Geofrey E. Mnzava Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa  2024 amepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa majisafi na salama wenye thamani ya shilingi milioni 601,868,971/= ambao unanufaisha wakaazi 4000 wa vijiji vya Ntalikwa, Tumbi, Kakola na Magoweko iliyosomwa na kuwasilishwa na Mhandisi Mayunga A. Kashilimu Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA.

Baada ya kufanya ukaguzi wa Mradi huu ameipongeza TUWASA kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa manunuzi ya umma (NeST) katika manunuzi ya vifaa vya mradi kwani mfumo huu umeongeza uthibiti na uwazi pia hakuna malalamiko kwakuwa wazabuni wote wanajipima kutokana na sifa zinazohitajika.

Ameendelea kueleza kuwa ni azma ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama maeneo ya karibu na hasa ukizingatia kuwa ni fedha nyingi zinatolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji.

Amesisitiza kuwa TUWASA na wananchi wote walioko maeneo ya miradi ya maji kuhakikisha wanalinda na kutunza miradi ya maji ili iendelee kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.

“Hapa sasa mradi huu wa majisafi na salama umekamilika tumepitia nyaraka zote na kutembelea mradi tumeridhika na sasa tunauzindua mradi huu “ Ndg. Godfrey Eliakimu Mnzava.