TUWASA YASHIRIKI KIKAO CHA WATUMISHI WA UMMA MANISPAA YA TABORA NA MWENYEKITI WA CCM MKOA

Watumishi wa Umma Manipaa ya Tabora wameshiriki kikao baina yao na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Ndg. Said Juma Nkumba (MNEC) kilichofayika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Tabora.
Ndg. Nkumba alieleza kuwa CCM inatambua, inapongeza na kuthamini kazi zote zinazofanywa na watumishi wa Umma Manispaa ya Tabora ikiwepo ujenzi wa barabara, upatikanaji wa huduma ya maji n.k ili kuhakikisha Ilani ya CCM inatekelezwa na kuleta tija kwa wananchi.
Kwa msisitizo amewataka watumishi wa Umma kufanya yafuatayo;-
- Waendelee kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma.
- Viongozi wote waendelee kuwa walezi wa watumishi wanaowasimamia na kujenga upendo.
- Watumishi wa Umma waepuke rushwa, uzembe kazini, kuchafuana na kuchafua Taswira ya Tabora mitandaoni.
Mwisho Bi Asha Churu ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Tabora akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Tabora alisema amepokea maelekezo yote na atasimamia watumishi wa Umma Manispaa ya Tabora waendelee kufanya kazi kwa weledi na kuendelea kuitangaza kwa wananchi miradi yote ya maendeleo ya Tabora.