TUWASA YAWASHIKA MKO...
TUWASA YAWASHIKA MKONO WATOTO KITUO CHA ISTIQAMA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.
10 Oct, 2025
TUWASA YAWASHIKA MKONO WATOTO KITUO CHA ISTIQAMA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

Baadhi ya Watumishi wa TUWASA wametembelea kituo cha kulea watoto cha Istiqama na kuwapatia chakula na vinywaji kama moja ya jukumu la msingi la kurudisha kwenye jamii.

Pia mfumo wa maji kwa ajili ya kunywa umeanza kujengwa kituoni hapo ili kuhakikisha watoto wanakunywa maji safi na salama kwa muda wote bila usaidizi wa viongozi wa hapo hasa ukizingatia kuwa watoto wapo wenye umri tofauti tofauti.

Hii ni katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo TUWASA ina utaratibu huu kila mwaka.

Bw. Rashid Yusuf ambaye ni Mkurugenzi msaidizi kituoni hapo ameushukuru uongozi wa TUWASA kwa kufanya jambo hili na amewaomba Taasisi na watu binafsi waige mfano huu wa TUWASA kusaidia watoto hao ambao wana mahitaji mengi.

Amehitimisha Bi. Khadija Bunduki ambaye ndiye Mkurugenzi wa Kituo kwa kushukuru sana uongozi wa TUWASA na hasa jambo la maji ya kunywa ambalo lilikuwa changamoto kubwa kwa watoto kituoni hapo.