WATUMISHI WA TUWASA WAPEWA MAFUNZO YA KUTUMIA MFUMO WA NeST- National e-Procurement System of Tanzania
Ndugu Yasri S. Mosha Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi TUWASA akishirikiana na wataalam wa Tehama kuwajengea uwezo watumishi wa TUWASA namna ya kutumia mfumo mpya wa Serikali wa Manununuzi NeST (National e- Procurement System of Tanzania).Mafunzo hayo yalikuwa na washiriki kutoka katika Kurugenzi ya Huduma kwa wateja, Kurugenzi ya usambazaji maji, Kurugenzi ya Rasilimali watu na Utawala, Kitengo cha Mkaguzi wa ndani na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma
Mkurugenzi huyo alieleza kwamba Mfumo huu unarahisisha masuala yote ya manununuzi kwa njia ya kielektroniki kama vile zabuni,mikataba, manunuzi ya bidhaa n.k. Aidha ameongeza kuwa mfumo huu utaboresha kazi za manununuzi katika upande wa kuharakisha taratibu na kwa ufanisi zaidi.
Amewaomba washiriki kuwa makini katika mafunzo hayo ili kujiandaa na matumizi ya Mfumo huu mpya kwa masuala yote ya kimanunuzi na endapo watapata changamoto wakati wa kuutumia wasisite kumuona kwa ajili ya msaada zaidi.