WATUMISHI WA TUWASA...
WATUMISHI WA TUWASA WAELIMISHWA KUHUSU SHERIA YA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA YA MWAKA 1995.
28 Jun, 2023
WATUMISHI WA TUWASA WAELIMISHWA KUHUSU SHERIA YA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA YA MWAKA 1995.

Ndugu Gerald A.  Mwaitebele Katibu msaidizi Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma pamoja na Ndugu Patric Shayo Afisa wa Maadili Kanda ya Magharibi wamewanoa watumishi wa TUWASA kuhusu maadili katika Utumishi wa Umma kwa kuwaelimisha kuhusu Sheria ya Maadili ya Utumishi wa Umma ya mwaka 1995, Maadili ya Utumishi wa Umma na Mgongano wa maslahi.

Viongozi hao wamewaelimisha watumishi wa TUWASA kuhusu uadilifu na kusaidia jamii yote kuwa waadilifu kupitia ngazi za familia ili kuimarisha usimamizi wa maadili kwa jamii nzima na pia  wamekumbushwa kuwa , maadili ni muhimu katika uwajibikaji kwa Umma.

Aidha watumishi wameaswa kutokuwa na mgongano wa maslahi ili kupata manufaa kinyume na Sheria na badala yake wazingatie mienendo ya kimaadili kwa kutoa huduma bora, Kutii Serikali, Kuwa na Bidii ya kazi, Kutoa huduma bila upendeleo na kuwa na matumizi sahihi ya Taarifa.

Pia wamekumbushwa kufuata utaratibu wa kupokea zawadi zinazozidi tshs 200,000 kuhakikisha wanaziwasilisha kwa Afisa Masuhuli kwa taratibu zilizoelekezwa ili kuepuka mtego wa kutofanya maamuzi kwa haki na kutozingatia Sheria.