TUWASA YAKAMILISHA M...
TUWASA YAKAMILISHA MCHANGO WA SHILINGI MILIONI 30 ZA UJENZI WA ZAHANATI KIJIJI CHA IGAMBILO, MISHA TABORA.
24 Jul, 2023
TUWASA YAKAMILISHA MCHANGO WA SHILINGI MILIONI 30 ZA UJENZI WA ZAHANATI KIJIJI CHA IGAMBILO, MISHA TABORA.

TUWASA imewasilisha kiasi cha shilingi milioni 14  na awali iliwasilisha kiasi cha shilingi milioni 16 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa zahanati Kijiji cha Igambilo kupitia utaratibu wa kurejesha kwa jamii (corporate social responsibility).

Eng. Mayunga Kashilimu  ameeleza kwamba kutokana na kuwa wananchi wa eneo la Igambilo wapo karibu na bwawa la Igombe na wanalilinda ni sababu kubwa ya kufanya jambo la kuchangia ujenzi wa Zahanati na hata watumishi wa TUWASA waliopo hapo watapata huduma za afya kwa urahisi zaidi.

Pia Ndugu Elias M. Kayandabila Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora amemshukuru Mkurugenzi wa TUWASA kwa mchango huo na amewaomba Taasisi na Mashirika mengine kuiga mfano huu kwakuwa jamii ina mahitaji mengi na hata Ofisi yake itaongeza fedha kuchangia ujenzi huo ili ukamilike na Zahanati ianze kutoa huduma kwa wananchi.

Mhe. Yassin Kushoka Diwani wa kata ya Misha ametoa shukrani nyingi kwa kuwakilisha wananchi wake wanaoishi Kijijini hapo kuhusu mchango huo wa shilingi milioni 30 na amemshukuru sana Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchangi shilingi milioni 50 za ujenzi wa zahanati hiyo.