TUWASA KATIKA MAONESHO YA NANENANE 2025 VIWANJA VYA IPULI TABORA.

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma zinazotolewa TUWASA katika maonesho ya Nanenane 2025 yanayofanyika kwenye viwanja vya Ipuli Tabora.
Elimu inayotolewa ni kuhusu utaratibu wa usomaji wa Dira za maji, maunganisho mapya, utunzaji wa mazingira pamoja na kupata ufafanuzi kuhusu maswali wanayouliza.
Pamoja na utoaji wa elimu TUWASA inatoa huduma ya maunganisho mapya na ankara za maji kwenye banda la Maonesho na kupokea maoni ya wateja kuhusu huduma za TUWASA.
Aidha Eng.Mayunga A. Kashilimu - Mkurugenzi Mtendaji TUWASA ametembelea banda la TUWASA, RUWASA na Bonde la Ziwa Tanganyika katika maonesho haya ya NaneNane.
“Chagua Viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025”.