TUWASA NA RUWASA WAPONGEZEZWA KWA UTEKELEZAJI MRADI WA MAJI KIGWA NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2024.
20 Aug, 2024
TUWASA NA RUWASA imepongezwa kwa utekelezaji wa mradi wa maji Kigwa ambao umefikia utekelezaji wa asilimia 72 hadi sasa na zimetumika fedha zaidi ya Bilioni 11 alieleza Eng. Godfrey Shibiti ambaye ni Meneja wa RUWASA Wilaya ya Uyui kupitia taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji Kigwa.
Baada ya mradi huo kukaguliwa umewekewa jiwe la msingi . "MRADI WA MAJI KIGWA KAZI IMEFANYIKA KAZI IMEONEKANA NA KAZI IENDELEE" Ndg Geofrey E. Mnzava kiongozi wa mbio za Mwenge 2024 .
Kauli Mbiu
Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu.