KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI CHA TATHMINI YA BAJETI YA MWAKA 2023/24 KIMEKETI TAREHE 25/09/2024.
Tarehe 25.09.2024 kimefanyika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kwa ajili ya tathmini ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24, ambapo pamoja na wajumbe waliohudhuria alikuwepo mwakilishi wa Wizara ya Maji Bi. Julia Benedictor na Mwakilishi kutoka TUGHE Taifa Bw. Avit Anicet.
CPA. Olimpia P. Maskini ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Hesabu aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/24 ambayo pamoja na changamoto zilizopo aliainisha mafanikio kama ifuatavyo:-
Wateja wapya 2324 wameungwa katika huduma ya majisafi, wateja 19 wa majitaka wameunganishwa katika huduma, mtandao wa km 16.3 wa majisafi umeongezwa pamoja na km 1.05 mtandao wa majitaka.
Wajumbe wameshauri matumizi ya mita za malipo kabla yapewe kipaumbele, juhudi za kuunga wateja wapya ziongezwe sambamba na kufuatilia madeni ya wasiolipa ingawa walipongeza wateja wa majumbani kwa ulipaji mzuri wa ankara za maji kwa wakati.
Aidha Mwakilishi wa TUGHE taifa (Wa pili kulia) amempongeza mwajiri kwa kushirikiana vema na chama cha TUGHE na pia kuendesha vikao hivi vya Baraza.
Mwenyekiti wa Baraza Eng. Mayunga Kashilimu (Aliyekaa Katikati) ambae ni Mkurugenzi Mtendaji - TUWASA amesema ataendelea kutoa ushirikiano katika chama cha TUGHE, pia amesema kuhusu mita za malipo ya kabla tayari zinafanyiwa kazi.
Amesisitiza ushirikiano baina ya watumishi ili kuhakikisha malengo yanayowekwa yanafikiwa kwa manufaa ya Taasisi na ya watumishi.