KAMATI YA USALAMA MK...
KAMATI YA USALAMA MKOA WA TABORA YATEMBELEA MRADI WA USAMBAZAJI MAJI MANISPAA YA TABORA KATIKA KATA YA NTALIKWA.
11 Sep, 2023
KAMATI YA USALAMA MKOA WA TABORA YATEMBELEA MRADI WA USAMBAZAJI MAJI MANISPAA YA TABORA KATIKA KATA YA NTALIKWA.

Kamati ya Usalama Mkoa wa Tabora ikiongozwa na Mhe. Dkt Batilda.S. Buriani (wa kwanza kulia) Mkuu wa Mkoa wa Tabora imetembelea mradi wa usambazaji maji Manispaa ya Tabora katika kata ya Ntalikwa kwa ajili ya kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kuingia Manispaa ya Tabora tarehe 15.09.2023.

Kamati imeridhishwa na maandalizi ya eneo hilo la mradi na kusisitiza kumalizia kazi ndogo ndogo zilizobakia kama vile kuzungushia uzio ili miti iliyopandwa isiharibiwe na kuendelea kufanya usafi eneo hilo.

Mradi huu umegharimu  kiasi cha shilingi milioni 601,868,971 na wananchi wameanza kunufaika na huduma ya majisafi na salama.

Eng. Juma Kasekwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA (anayesoma taarifa) amepokea maelekezo yote na kuahidi kuyafanyia kazi kwa kushirikiana na menejimenti kabla Mwenge wa Uhuru haujafika.