KAMATI YA SIASA YA M...
KAMATI YA SIASA YA MKOA WA TABORA IMEKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA MAJI AMBAPO IMETEMBELEA MRADI WA MAJI WILAYA YA KALIUA
11 Dec, 2023
KAMATI YA SIASA YA MKOA WA TABORA IMEKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA MAJI AMBAPO IMETEMBELEA MRADI WA MAJI WILAYA YA KALIUA

Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Tabora imekagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika sekta ya maji ambapo imetembelea mradi wa Maji Kaliua wenye tenki la ujazo wa lita 50,000.

Eng. Mayunga Kashilimu Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA ameeleza utekelezaji wa Ilani kwamba kwa sasa ni asilimia 25 tu ya wakazi wa Kaliua wanapata majisafi kutokana na changamoto ya maji kwakuwa wanatumia maji ya visima.

Pia ameeleza kwamba changamoto hii itakwisha mara baada ya mradi wa kuleta maji ya Ziwa Victoria Kaliua kupitia mradi unaotekelezwa ambao umefikia asilimia 26.

Mradi huu utakamilika mwezi Octoba, 2025 na asilimia 95 ya wakazi wa Kaliua watapata majisafi kwa mujibu wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Kamati imesisitiza utekelezaji wa mradi huu ufanyike haraka ili wananchi wapate majisafi kwakuwa asilimia ndogo sana ya wakaazi wa Kaliua ndio wanapata majisafi.

TUWASA imepewa kusimamia Mji wa Kaliua kwa kata tatu za Ufukutwa, Ushokola na Kaliua kupitia Tangazo la Serikali namba 788 la Tarehe 03 Novemba, 2023.