KAMATI YA KUDUMU YA...
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE UWEKEZAJI MITAJI YA UMMA (PIC) YATEMBELEA MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TABORA NA KUKAGUA MRADI WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA
23 Mar, 2023
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE UWEKEZAJI MITAJI YA UMMA (PIC) YATEMBELEA MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TABORA NA KUKAGUA MRADI WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA

Kamati ya kudumu ya bunge uwekezaji mitaji ya umma (pic) yatembelea Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora na kukagua mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria .

Tarehe 16.03.2023 na kuridhishwa na namna ambavyo Mradi huo unafanya kazi, Aidha Kamati hiyo ilipokea taarifa ya Mradi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA Mhandisi Mayunga Antony Kashilimu na baadaye kutoa maelekezo yafuatayo;

  • Bodi na Menejimenti ya TUWASA kuhakikisha inaongeza wateja wapya
  • Kuhakikisha inapunguza upotevu wa maji kutoka 27% hadi 20% kwa kudhibiti wizi wa maji na kubadilisha mabomba chakavu
  • Kuhakikisha kunakuwa na mpango wa kukusanya fedha za Taasisi za Serikali baada ya kutumia huduma ya maji kila mwezi
  • Kuhakikisha kunakuwa na mpango wa dhati wa uwekezaji kwa kutumia fedha za makusanyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya TUWASA Bw. Dick Mlimuka aliyapokea maelekezo ya Kamati na kuahidi kuisimamia Menejimenti kwa ajili ya kuyatekeleza kwa ufanisi.