BODI YA TISA (09) YA...
BODI YA TISA (09) YA WAKURUGENZI TUWASA IMEKETI KIKAO CHAKE CHA KWANZA KUJADILI TAARIFA YA UTEKELEZAJI
31 Oct, 2023
BODI YA TISA (09) YA WAKURUGENZI TUWASA IMEKETI KIKAO CHAKE CHA KWANZA KUJADILI TAARIFA YA UTEKELEZAJI

Leo Tarehe 31.10.2023 Bodi ya tisa ya Wakurugenzi TUWASA imeketi kikao chake cha kwanza na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu hasa ikiwepo hali ya uzalishaji na usambazaji maji manispaa ya TABORA.

Ameeleza Eng Mayunga Kashilimu ambaye ni katibu wa Bodi ya wakurugenzi kwamba umeme unasababisha huduma kutokuwa ya kutosha lakini tayari mazungumzo yamefanyika TANESCO ili kuona namna ya kuwa na umeme katika chanzo cha Igombe na Kazima hali ambayo italeta nafuu kubwa ya huduma ya maji manispaa ya Tabora.

Ameendelea kueleza kuhusu kupungua kina cha maji  bwawa la Utyatya Sikonge na juhudi zinazofanyika ikiwepo kuangalia uchimbaji wa visima ili kuongeza upatikanaji wa maji Sikonge.

Bodi ya wakurugenzi imepokea taarifa hiyo na kuagiza menejimenti ihakikishe inafanyia kazi jambo hili kidharura.