WAZIRI WA MAJI AMHAK...
WAZIRI WA MAJI AMHAKIKISHIA MHE. RAIS UPATIKANAJI WA MAJISAFI NA SALAMA YA KUTOSHA MKOA WA TABORA.
18 Oct, 2023
WAZIRI WA MAJI AMHAKIKISHIA MHE. RAIS UPATIKANAJI WA MAJISAFI NA SALAMA YA KUTOSHA MKOA WA TABORA.

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya Ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora ambapo ametembelea Wilaya ya Igunga na Nzega katika miradi mbalimbali ikiwepo miradi ya Maji.

Pia Mhe. Jumaa H. Aweso Waziri wa Maji, ameeleza kuwa katika Mkoa wa Tabora tatizo la maji lilikuwa sugu sana lakini kwa sasa hali ni nzuri kwakuwa upatikanaji wa maji umefikia asilimia 98 mijini ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa katika Wizara ya maji kuhakikisha maji yanapatikana kwa asilimia 95 mijini na vijijini asilimia 85 ifikapo mwaka 2025.

Ameendelea kueleza kwamba mkakati uliopo wa Wizara ya maji ni kuhakikisha maji ya Ziwa Victoria yanafika katika Wilaya zote za Tabora ambapo kwasasa ili kulitimiza hilo wakandarasi wako site Sikonge, Urambo na Kaliua.

Mwisho kabisa amemuhakikishia Mhe. Rais kuwa yeye pamoja na timu nzima ya Wizara ya Maji hawatokuwa kikwazo kwa Mkoa wa Tabora kupata majisafi na salama yenye kutosheleza.