Mkurugenzi mtendaji wa TUWASA ameshiriki mapokezi ya Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
09 Oct, 2024

Eng. Mayunga A. Kashilimu - Mkurugenzi mtendaji wa TUWASA ameshiriki mapokezi ya Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mapokezi yamefanyika Wilaya ya Igunga ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo wilaya za Nzega na Igunga imewekewa mawe ya Msingi na Mhe. Dkt Philip Mpango.
Ziara hii itaendelea katika wilaya zingine Mkoani Tabora kwa ajili ya kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwepo mradi mkubwa wa maji wa miji 28 wenye thamani ya shilingi Bilioni 145 kupeleka maji Sikonge, Urambo na Kaliua ambao unatarajiwa kukamilika Oktoba, 2025.