BODI YA 9 YA WAKURUG...
BODI YA 9 YA WAKURUGENZI TUWASA IMETEMBELEA MRADI WA MAJI WA MIJI 28 WA KUPELEKA MAJI SIKONGE, URAMBO NA KALIUA.
30 Oct, 2023
BODI YA 9 YA WAKURUGENZI TUWASA IMETEMBELEA MRADI WA MAJI WA MIJI 28 WA KUPELEKA MAJI SIKONGE, URAMBO NA KALIUA.

Eng. Mayunga Kashilimu Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA, ameieleza Bodi kuwa mradi huu unagharimu fedha kiasi cha bilioni 143.26 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Octoba, 2025 na utamaliza changamoto ya upatikanaji wa maji wilaya za Sikonge , Urambo na Kaliua.

Aidha Wakurugenzi wa Bodi wametembelea mradi wa majitaka wenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 unaotekelezwa eneo la Milambo Barracks pamoja na tenki la maji la Itumba na Kazehill ili kuona namna maji yanavyosafirishwa kuja matenkini na kusambazwa kwa wateja.

Mwisho Bodi ilitembelea chanzo cha maji cha Igombe ambacho kinazalisha asilimia 60 ya maji kwa wakaazi wa manispaa ya Tabora.

Ziara hii ilikua ni ya mafunzo kwa Bodi hii mpya ili kuielewa Mamlaka na uendeshaji wake na kabla ya ziara wajumbe walipewa taarifa ya Mamlaka iliyohusisha mambo yote muhimu ikiwepo uzalishaji wa maji, usambazaji, mapato na makusanyo, eneo linalohudumiwa na TUWASA ambalo ni Tabora manispaa, Isikizya, Sikonge, Urambo na Kaliua, changamoto, uendeshaji na hasa utekelezaji wa miradi iliyopo yenye lengo la kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira.